Sina Kinyongo na Wala Sijaumia Belle 9 Kuoa- Lulu Diva

Akizungumza na Mikito Nusunusu baada ya kuenea minong’ono ya wambea wa jiji kwamba kitendo cha Belle 9 kufunga ndoa kitakuwa kimemuumiza mrembo huyo alisema, hajaumia hata kidogo sababu kwa sasa Belle 9 ni rafiki yake wa karibu wala hawazi tena mambo ya mapenzi.
“Ni kweli niliwahi kuweka wazi hisia zangu kwamba namzimikia enzi hizo, lakini hayo yalipita Belle 9 tunaheshimiana kama marafiki tu, pia nashukuru alinialika kwenye harusi yake lakini mambo yalinibana nikashindwa kwenda, kikubwa nampongeza kufunga pingu za maisha,”alisema.
No comments