Techno Yawaandalia wadau wake Hafla ya KRISIMASI
Katika
kusherehekea sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya, kampuni ya simu
TECNO mobile Ltd imeandaa sherehe za awali za Krisimasi maalumu kwa
wadau wake.
TECNO
iliwakutanisha wadau na mashabiki wake kutoka katika mitandao ya
kijamii mbalimbali ikiwemo, Twitter, Instagram, Facebook na TECNO spot
katika hafla fupi iliyopewa jina la “TECNO Fans Night” iliyofanyika
katika uwanja wa burudani wa ESCAPE ONE Mikocheni.
Kusudio
likiwa ni kuwapongeza na kutoa shukurani kwa wadau na mashabiki kwa
kuwa pamoja na kampuni hiyo kwa mwaka mzima na kuwa mabalozi wa kampuni
hiyo ya simu.
Sherehe
hiyo ilikua na ugeni wa mtangazaji maarufu afahamikae kwa jina la “Lil
Ommy” Omary Tambwe wa Times FM akiwa kama shereheshaji wa sherehe hiyo
iliyoandaliwa na TECNO. Hafla hiyo ilipambwa kwa michezo, burudani na
chakula cha jioni huku zawadi mbalimbali zikitolewa kwaaajili ya
mshabiki na wadau wa kampunI hiyo ya TECNO waliofika.
“Kiukweli
nimefurahi kuwa hapa, kuungana na wenzangu. Nimepata nafasi ya kuongeza
marafiki usiku wa leo, asante sana TECNO” – alisema mmoja wa
wadau/shabiki wa TECNO.
“Mpaka
sasa kwa mwaka huu tumeweza kuwa na ushawishi sana kwa upande wa
mitandao ya kijamii na tumeweza kuwapa kile wadau na mashabiki wetu
wanapenda, nahisi ndicho kilichoweza kutupa mabalozi kama hawa. Kiukweli
hatuwezi kuwa sisi bila ya watu kama hawa ambao waipenda bidhaa na
kampuni hivi, hivyo ni sawa tu kama na sisi kama kampuni tukatenga muda
ili kuweza kuungana nao kusherehekea mafanikio na pia sikukuu” – Meneja
mahusiano.
TUNAWATAKIA KHERI YA KRISIMASI
Tazama video ya yaliojiri kupitia


