Vyuma vimelainika Kinondoni - Meya Sita

Kushoto ni meya wa Kinondoni akikabidhi mfano hundi ya milioni 10 kata ya Ndugumi
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, leo imezindua awamu ya kwanza ya utoaji wa asilimia 10 kwa vikundi vya ujasiriamali vya vijana na akina mama ambapo jumla ya sh.bilioni 2.3 zitatolewa.
Katika hafla hiyo ya uzinduzi huo ambao umefanyika jijini Dar es Salaam, ambapo manispaa hiyo imetoa hundi zenye thamani ya pesa taslimu za kitanzania Tsh.milioni 200 kwa vikundi 154.
Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hizo, Meya wa Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Sitta amesema kuwa, mwaka wa fedha 2017/18 manispaa hiyo imetenga kiasi hicho cha fedha ili kuwawezesha vijana na akina mama kuweza kukoka ili kuinuka kiuchumi.
Aidha Meya Sitta alitoa rai wananchi wa Kinondoni hususani vijana kuacha tabia ya kulalamika vijiweni na kusema vyuma vimekaqza, badala yake wafanye kazi au kuunda vikundi ambavyo vitawasaidia kupata kipato na pia kuweza kupata mikopo ambayo inatolewa na manispaa hiyo kwa ajili yao kwani fedha za kutosha zipo na zimeletwa na zimetengwa kwa niaba yao.
''Tunatoa fedha hizo kwa watu wanaokopesheka na waliokizi vigezo vya kupata mkopo kwani tumefanya taathimini kwa kila kikundi hivyo leo kila kikundi kitapata fedha kwa ajili ya kuinua biashara zao'' alisema

Kushoto ni meya wa Kinondoni akikabidhi mfano hundi ya milioni 10

No comments