Olivier Giroud ampiga busu katika paji la uso Emmerson baada ya mchezaji
huyo kumpigia pasi murua iliomfanya kufunga bao lake la kwanza akiwa
Chelsea
Olivier Giroud na Willian waliisaidia timu ya Chelsea kuicharaza Hull
City mabao manne na hivyobasi kufika katika robo fainali ya kombe la FA
na sasa Mkufunzi wa klabu hiyo Antonio Conte anasema kuwa wamempatia
sababu njema kuhusu mechi kati ya timu hiyo na Barcelona.
Willian alionyesha mchezo mzuri katika mechi yote na alifunga bao la
kwanza kwa kuupinda mpira katika kona ya goli akiwa nje ya eneo hatari.
Pedro alifunga bao la pili baada ya kumchenga David Marshall kufuatia
pasi nzuri kutoka kwa Cesc Fabregas kutoka katikati ya uwanja.
Willian alifunga bao la tatu kutoka maguu 25 baada ya kucheza nipe nikupe na Giroud .
Mshambuliaji huyo wa Ufaransa baadaye alifunga bao lake la kwanza tangu
uhamisho wake kutoka Arsenal akiwa karibu na goli kufuatia krosi
iliopigwa na Emerson Palmieri kutoka wingi ya kushoto.
Chelsea watawajua wapinzani wao wa kombe la FA siku ya Jumamosi.
Baadye watachuana na Bercalona siku ya Jumanne katika robo fainali ya klabu bingwa Ulaya.
Conte alisema kuwa ilikuwa mechi nzuri baada ya Olivier Giroud kufunga huku Willian akionyesha mchezo mzuri.
''Kwa kweli nikienda nyumbani sasa nitakuwa na chaguo kwa kuwa wachezaji
wengi wamethibitisha kwamba viwango vya vya mchezo wao viko juu
No comments