Mambo bado ni mazito kwa ile couple iliyokuwa na nguvu mjini, Diamond na
Zari. Baada ya Zari kutangaza kumbwaga muimbaji huyo drama zimekuwa
zikiendele bila kusimama.
Zari The Boss Lady ametumia mtandao wa Snapchart kuweka video ambayo
unasikika wimbo wa Diamond uitwao Sikomi kisha kuweka caption
iliyosomeka ‘Utakoma tu mwenzangu’
Hapo jana Diamond pia aliweka video ya ngoma hiyo katika mtandao wa
Instagram na kuandika; ‘Unajua Nyimbo zingine Unaziimba ila Hata we
mwenyewe zinakuingia Baadaye’.
Jumatano ya wiki hii katika siku ya wapendanao (Valentine’s Day) Zari
The Boss Lady alitangaza rasmi kuachana na Diamond kutokana na kuchoshwa
na habari za kusalitiwa ambazo husikika kila siku katika vyombo vya
habari. Katika mahusiano yao Diamond na Zari wamefanikiwa kupata watoto
wawili ‘Tiffah na Nillan’.
No comments