Mheshimiwa Hashim Rungwe Spunda Mwenyekiti (CHAUMMA) jana Februari 15,
2018 aliungana na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kumnadi
mgombe Ubunge wa CHADEMA katika jimbo la Kinondoni Salum Mwalimu.
Akiwa kwenye mkutano huo ambao ulifanyika katika Kata Ya makumbusho
Viwanja Vya Vegas Rungwe alisema kuwa wana Kinondoni hawapaswi kumchagua
mgombea wa CCM kwa kuwa ni msaliti na amekuwa muongo.
"Serikali hii ya CCM inajidai sanaa inafanya propaganda kwenye Radio na
kila mahali lakini mimi naomba niulize wangapi wamekuja hapa hawana kitu
mfukoni, mna hela nyie? Wananchi hali zao mbaya watu hawana kitu.
Jamani tunampima kiongozi kwa mambo anayofanya tumeona tawala nyingi
lakini mmeshawahi kuona utawala wa namna hii? Yaani polisi ndiyo
wanafanya serikali ifanye kazi yaani bila ya polisi hawafanyi kazi,
polisi ndiyo wamewekwa mbele yaani ukisema hivi unakamatwa"
Rungwe aliendelea kuelezea juu ya sakata lake la kukamatwa na polisi siku za karibuni
"Mnakumbuka mimi nilikamatwa juzi juzi hapa yaani hakuna kitu chochote
cha maana mpaka sasa mimi ni Wakili na Wakili kazi yake ni kusaini
nyaraka, nimesaini nyaraka za watu na hao watu wenye pesa walikuwa
wakitoa maagizo mlipe huyu na huyu na mimi nalipa sasa mimi nimefanya
kosa gani? Hawa watu ni wabaya na haya ni mambo ya serikali ya CCM,
hakikisheni kwamba serikali ya CCM mnaiondoa msikubali Mtulia awe Mbunge
wenu. CCM ndiye wanaiharibu nchi hii" alisisitiza Rungwe
No comments