Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano ndani ya klabu ya Simba Haji
Manara amesema Simba sio timu ya kwanza kutoa sare au kufungwa na Mwadui
hivyo mashabiki wasiongee sana.
Kupitia moja ya kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii Manara ameandika
ujumbe ambao unaonekana kuwa povu kwa mashabiki wa wapinzani wao huku
akiweka wazi kuwa sare ya jana dhidi ya Mwadui FC kamwe haijaitoa Simba
kwenye njia.
''Simba haitatoka mstarini na washabiki wetu tulieni na wajibu wenu ni
kuiombea timu na kuisuport'', ameandika Manara ikiwa ni chini ya siku
moja tangu timu hiyo itoe sare ya 2-2 dhidi ya Mwadui ugenini Shinyanga.
Aidha Manara ameongeza ''Mwadui imezifunga Singida United na kabla yetu
sisi waliwafunga Mtibwa 3-1 kule Shinyanga, wametoka sare na Yanga na
Azam tena wakiwa kwao Dar, hizo ndio 'big five' kwenye ligi kwa sasa,
sisi kutoka nao sare kwao 'why' iwe nongwa tena ugenini'', ?.
Baada ya sare ya jana Simba imefikisha alama 42 ikiwa kileleni kwa alama
5 zaidi ya Yanga ambayo inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 37 huku
Azam FC ikishika nafasi ya tatu ikiwa na alama 34.
No comments