Kesi ya Tido Mhando yahairishwa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi ya
kusababisha hasara ya Shilingi Milioni 887 inayomkabili liyekuwa
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Tido Mhando hadi
February 28,2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (Ph).
Mwendesha Mashtaka wa (TAKUKURU), Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi
Mfawidhi, Victoria Nongwa kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya
kumsomea Tido maelezo ya awali.
Hata hivyo, Wakili wa Tido, Ramadhan Maleta ameieleza Mahakama kuwa
amechelewa kumuandaa mteja wake kutokana na kuchelewa kupewa maelezo ya
(Ph), hivyo anaomba ahirisho.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi February 28,2018 kwa ajili ya Tido kusomewa (Ph).
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka Tido anakabiliwa na makosa matano ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.
Inadaiwa alilitenda kosa hilo June 16,2008 akiwa Dubai kama mtumishi wa
TBC alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mikataba ya uendeshaji wa
vipindi kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BVI) bila kutangaza
zabuni na kuisababishia channel hiyo kunufaika.
Inadaiwa kati ya June 16 na November 16,2008 akiwa Falme za Kiarabu,
kama muajiriwa wa TBC kwa cheo cha Mkurugenzi Mkuu kwa mamlaka yake
alilisababishia shirika la TBC hasara ya Sh.Mil 887.

No comments