Header Ads

Milioni 50 zamtoa Mhe. Zitto Kabwe mahabusu

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe ameachiwa na Polisi kwa dhamana yenye thamani ya Tsh milioni 50 asubuhi hii mjini Morogoro baada ya kulala mahabusu tangu jana Alhamisi Februari 22, 2018  usiku.
Zitto Kabwe
Taarifa hizo zimethibitishwa na Wakili wa Mbunge huyo wa Kigoma Mjini, Ndg Emmanuel Mvula ambaye ndiye aliyemdhamini Zitto Kabwe na kusema kuwa anatakiwa kuripoti katika kituo kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro siku ya Jumatatu Machi 12, 2018.

Mhe. Zitto Kabwe alikamatwa jana Februari 22, 2018 na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro wakati akiwa katika ziara ya Chama cha ACT Wazalendo inayoendelea kufanywa na chama hicho katika mikoa 8 Tanzania bara.

No comments

Powered by Blogger.