Mabalozi Walioapishwa Jana (Dr Salaa na Muhidin Ally) Wamuaga Makamu Wa Rais Leo
Balozi
wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Ally Mboweto pamoja na Balozi
wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Wilbrod Peter Slaa leo wamekutana na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan kwenye makazi yake Oysterbay, jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kumuaga tayari kwenda kwenye vituo vyao vipya vya kazi.
Mabalozi hao waliapishwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar Es Salaam .
Makamu
wa Rais aliwatakia safari njema huko waendapo kwenye vituo vipya vya
kazi ambapo aliwasihi kwenda kufanya kazi kwa moyo mmoja na kuzingatia
maelekezo ya Mhe. Rais
“Hakikisheni
mnaitangaza nchi yetu vizuri na kuwashawishi wawekezaji ili waweze
kuja kwa wingi, nchi yetu ina fursa za kutosha” alisema Makamu wa Rais.
Kwa upande wao Mabalozi hao walimuahidi Makamu wa Rais kuiwakilisha nchi vizuri na kufanya kazi kizalendo.


No comments