SKENDO iliyomganda msanii wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha
ni ya kushindwa kulipa kodi kwenye nyumba aliyokuwa akiishi awali na
kuhamia kwa ‘shogaake’ Issabela Mpanda ‘Bela Fasta’ maeneo ya Mbezi
Beach.
Madai ya awali yalieleza kuwa, mambo sasa hivi yamemuendea kombo staa
huyo kiasi cha mkwanja kumpitia pembeni, mazingira yaliyomfanya ashindwe
kwenye baadhi ya mahitaji muhimu likiwemo hilo la kodi ya pango.
Kufuatia madai hayo, paparazi wetu alimtafuta Madaha na alipopatikana alishangazwa na madai hayo na kusema:
“Hayo ni maneno ya watu wenye chuki na mimi. Si kweli kwamba nimefulia.
Na ifahamike kwamba siku nyingi nakuwa niko Dubai ambako nafanya
shughuli zangu, ninapokuja huku Bongo kufikia kwa Bela siyo tatizo.
“Nilirudi hivi karibuni kwa ajili ya harusi ya mdogo wangu na siishi
hapa kwa hiyo suala la kushindwa kulipa kodi na kwenda kuishi kwa Bela
halina mashiko!
No comments