Header Ads

Idadi ya vifo yaongezeka Burkina Faso


Idadi ya vifo vya askari kutokana na shambulizi lililotokea katika mji mkuu wa Ouagadougou nchini Burkina Faso imeongezeka mpaka 8.

Kwa mujibu wa habari,rais Roch Marc Christian Kabore amezungumza kuhusu shambulizi hilo katika vyombo vya habari na kusema kuwa nchi yake imevamiwa na wapiganaji wahalifu walioshambulia na kusababisha vifo vya askari wa nchi hiyo.

Rais Roch Marc Christian Kabore ametoa salamu za rambirambi kwa familia zote zilizoguswa na shambulizi hilo.

Ameahidi pia kuendelea kusimama wima katika kupambana na ugaidi nchini humo.

Mashambulizi hayo yalifanywa karibu na wizara kuu pamoja na UN.

No comments

Powered by Blogger.