Watu wawili wamekatwa na kufungwa jela baada ya kumchezea rafu Rais wa
Burundi, Pierre Nkurunzinza katika mchezo wa kirafiki uliokuwa dhidi ya
timu yake na wapinzani.
Nkurunzinza ambaye alikuwa na kikosi chake cha Haleluya FC, Februari 3
2018 walikuwa wakicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kimbere FC iliyopo
Kaskazini mwa nchi hiyo ya Burundi.
Katika mchezo huo, Kiremba FC ilikuwa na wachezaji ambao baadhi ni
wakimbizi kutoka Congo waliokuwa hawajui kama wanacheza na Rais wa
Burundi hivyo walikuwa wakimchezea rafu kila muda.
Kitendo cha kumchezea rafu Rais huyo, kilichukuliwa kama njama za kutaka
kuhatarisha afya ya Rais Nkurunziza hivyo Serikali ikachukua maamuzi ya
kuwafunga jela.
No comments