Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameitaka bodi ya barabara
kuhakikisha fedha za Mkopo wa Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara DMDP
zinatumika kujenga Barabara za kisasa na sio kutumika kwenye Warsha,
Semina na Safari za Mafunzo Nje ya Nchi ambapo Mwisho wa siku fedha hiyo
inamalizika bila kufanya jambo lililokusudiwa.
Makonda amesema Dar es salaam ina fedha za DMDP takribani Billion 600
kwaajili ujenzi wa Barabara na Mifereji ya Maji lakini asilimia kubwa ya
fedha hizo zimekuwa zikitumika kwenye semina na Safari za Nje ya Nchi
kujifunza namna ya usimamizi wa Barabara jambo linalopelekea Serikali
kulipa madeni kwa miradi ambayo haijatekelezwa.
Aidha Makonda amesema kuwa amegundua gharama ya kujenga Barabara ya
Kilometa moja kwa fedha ya DMDP ni sawa na gharama ya kujenga barabara
ya TANROAD Kilometa 3 hivyo ameshauri kikao hicho kuangalia kwa umakini
jambo hilo ili fedha hizo ziweze kuleta tija kwa wananchi kwa uwepo wa
barabara zenye ubora.
Makonda amesema kwa mwaka wa fedha wa 2018-2019 Mkoa wa Dar es salaam
umetenga kiasi cha shilingi Billion 289.3 kwaajili ya matengenezo ya
barabara kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo Wakala wa Barabara za Mjini na
Vijijini TARURA, TANROAD na vyanzo vya ndani vya Halmashauri.
Makonda amesema hataki kuona Wananchi wa Dar es salaam wanateseka
kutokana na ubovu wa barabara zenye Mashimo na mahandaki jambo
linalopelekea hasara ya uharibifu wa vyombo vya usafiri na wakati
mwingine ongezeko la msongamano wa magari.
Aidha Makonda ameanza kuona nuru baada Wakandarasi wa barabara za Dar es
salaam kuanza kufuata taratibu kwa kutengeneza barabara za kisasa na
kuwasihi TARURA wawe wasimamizi wazuri wa Ujenzi Barabara Kama
wanavyofanya TANROAD ili tuwe na barabara zinazodumu muda mrefu.
No comments