Neymar atengewa mamilioni ya fedha na NIKE endapo atashinda mataji haya
Haina ubishi kuwa mshambuliaji wa klabu ya PSG, Neymar Jr sasa yupo tayari kuandikwa kwenye orodha ya wachezaji wa soka matajiri zaidi duniani, na hii inadhihirika pale ambapo makampuni makubwa duniani yakijitokeza kumpa madili makubwa ya matangazo.
Neymar Jr
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Nike wamesema watampa Neymar kiasi cha Euro £720,000 sawa na Tsh bilioni 1.9 za kitanzania kama bonus kwenye mkataba wake kila mwaka kuanzia mwaka huu endapo mchezaji huyo atashinda tuzo ya Ballon d’Or .
Achana na hiyo, Nike wamesema endapo Neymar atabeba kombe la dunia mwaka huu watampatia bonus ya £36,000 sawa na Tsh milioni 99 kwenye mkataba wake.
Kama hiyo haitoshi, Neymar atapewa bonus ya Euro £144,000 sawa na Tsh milioni 399 endapo ataibuka mfungaji bora wa michuano ya kombe la dunia la mwaka huu.
Hata hivyo bado hela hizo zikawa bado ni kitendawili kwa Neymar, kwani hadi sasa yupo kwenye matibabu na timu yake inaingia kesho uwanjani kucheza na Real Madrid kwenye mchezo wa marudiano wa klabu bingwa. Ambapo kwa mujibu wa baba yake, Neymar atakaa nje ya uwanja kwa miezi mitatu.
Neymar (26) kwenye mkataba wake na Kampuni ya Nike anapokea kiasi cha Euro milioni £40 kwa mwaka na mkataba wake unaisha mwaka 2022.
No comments