Header Ads

Pakistan inatarajia kufanya uchaguzi mkuu ifikapo 25 mwezi Julai

Pakistan inatarajia kufanya uchaguzi mkuu ifikapo 25 mwezi Julai baada ya kupitishwa na rais Mamnoon Hussain.

Mhula wa miaka mitano wa serikali ya Pakistan na bunge lake unatarajia kufikia kikomo mnamo 31 Mei.

Baada ya hapo serikali ya muda mfupi itachukua nafasi ili kusaidia kufanyika kwa uchaguzi.

Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo,waziri mkuu na kiongozi wa upinzani huchagua waziri mkuu wa muda katika bunge.

Hata hivyo mpaka sasa chama tawala cha PML-N na chama cha upinzani havijaweza kumchagua waziri huyo.

No comments

Powered by Blogger.