DK. MPANGO atoa neno kuhusiana na uchumi wa nchi
Uchumi wa Tanzania umekua kwa kasi zaidi na kuzipita nchi zote za Ukanda wa Afrika Mashariki katika kipindi cha mwaka 2017.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango wakati akiwasilisha Hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2018/19.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, Uchumi wa Tanzania ulikuwa kwa kasi zaidi, ikilinganishwa na nchi nyingine katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa wastani wa asilimia 7.1, ikifuatiwa na Rwanda asilimia 6.1, Kenya 4.8, Uganda 4.5, na Burundi asilimia 0.0 ambapo uchumi wa Sudan Kusini ulipungua kwa asilimia 11.1,” alisema Dkt. Mpango.
Waziri alisema kuwa uchumi wa nchi hizi utaendelea kukua kwa kasi zaidi kufikia wastani wa asilimia 3.6 mwaka 2018 ikilinganishwa na mwaka 2016 ambapo ulikuwa kwa wastani wa asilimia 1.9.
Ongezeko la kasi ya ukuaji litatokana na maboresho yanayoendelea kufanyika katika sera na taratibu za uwekezaji na uendeshaji wa biashara, utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ya uimarishaji wa miundombinu ikiwemo miradi ya bomba la mafuta ghafi toka Hoima (Uganda) hadi banadari ya Tanga na ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Standard Gauge ambayo inaunganisha Tanzania, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi na Uganda.
Kwa mujibu wa Dkt. Mpango, Pato halisi la Taifa kwa Mwaka 2017 limeongezeka na kufikia Shilingi milioni 50.5 ikilinganishwa na Shilingi milioni 47.2 mwaka 2016, ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 7.1 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 7.0 kwa mwaka 2016.
Dkt. Mpango amesema kuwa ukuaji huo unatokana na jitihada za Serikali katika utekelezaji wa miradi ya miundombinu, kuongezeka kwa uzalishaji wa baadhi ya madini na kuimarika kwa sekta ya kilimo.
Dkt. Mpango amesema kuwa ukuaji huo unatokana na jitihada za Serikali katika utekelezaji wa miradi ya miundombinu, kuongezeka kwa uzalishaji wa baadhi ya madini na kuimarika kwa sekta ya kilimo.
Aliongeza kuwa katika kipiondi husika, shughuli za uchumi zilizokuwa kwa kasi kubwa ni: Uchimbaji wa madini na mawe, Usambazaji maji, Uchukuzi na uhifadhi mizigo, Habari na Mawasiliano na Ujenzi.

No comments