Jaji Lubuva apata uteuzi mwingine kutoka kwa JPM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Jaji Mstaafu, Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Taarifa kutoka Ikulu iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imsema kuwa uteuzi wa Jaji Lubuva umeanza leo Juni 18, 2018.
Jaji Mstaafu Lubuva anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. Peter Ngubullu.
Jaji Lubuva alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) 2015.

No comments