Header Ads

Manyika Jr kuhamishwa Singida na Baba yake


Baba wa kipa wa Singida United, Manyika Peter ambaye ni Peter Manyika, leo amepanga kuiandikia timu ya mwanaye barua ya kusitisha mkataba wa kuendelea kuichezea.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni siku chache tangu usajili wa Ligi Kuu Bara ufunguliwe kwa klabu 20 shiriki za ligi katika msimu ujao huku mwanaye akiwa amebakiza mwaka mmoja, ambapo amesema klabu hiyo imeshindwa kufuata makubaliano.

“Kuna makubaliano mengi yameshindwa kutimizwa kwenye mkataba wa mwanangu Manyika pamoja na klabu yake anayoichezea ya Singida, hivyo kama baba ambaye mimi ni meneja wake ninayemsimamia katika soka, nimeona nichukue maamuzi ya kuiandikia timu yake ya Singida barua ya kusitisha mkataba wake”, amesema Manyika.

Kipa huyo alijiunga na Singida msimu uliomalizika akitokea Simba baada ya mkataba wake kumalizika.

No comments

Powered by Blogger.