Magaidi 26 washambuliwa katika operesheni Qandil
Jeshi la Uturuki limeendeleza mashambulizi yake dhidi ya magaidi Qandil na kuangamiza magaidi 26.
Kwa mujibu wa habari,magaidi hao 26 wameangamizwa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na wanajeshi hao.
Uturuki ilianzisha operesheni dhidi ya magaidi wa PKK Qandil toka 12 Juni.
Toka kuanzishwe operesheni hiyo magaidi na ngome zao zimekuwa zikiangamizwa hapa na pale.
Uturuki imeahidi vita dhidi ya magaidi karibu na mipaka yake.

No comments