Header Ads

Mkuu wa mkoa wa manyara aipiga mkwara mamlaka ya maji babati bawasa

Na John Walter- Manyara
Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexender Mnyeti ameishauri mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira mjini Babati [BAWASA]kupanga miundo mbinu ya maji upya ili kutenganisha Magereza na nyumba za askari.

Mnyeti amesema hataki kusikia katika taasisi nyeti kama Magereza maji yanakatwa kisa madeni  huku akitishia kuifuta BAWASA na kuleta Mamlaka nyngine isimamie.

Ametoa agizo alipotembelea magereza ya mkoa iliyopo Mtaa wa Mrara Babati mjini ambapo alikuta maji yamekatwa Magereza kwa takribani siku tatu pamoja  na nyumba za askari kutokana na deni kubwa wanalodaiwa na BAWASA zaidi ya shilingi milioni 130.

Mnyeti amesema kweli Mamlaka hiyo inaidai Serikali lakin i kitendo cha kukata maji sio cha uungwana kwa sababu deni lipo.

Ni kweli BAWASA wanadai lakini kwanini wakate maji nani amewaambia wafanye hivyo? alihoji Mnyeti.

Akijibu hilo mhandisi wa BAWASA Rashidi Chalahani amesema ni wiki iliyopita walikuwa na kikao na uongozi wa Magereza kuhusu wamefikia wapi kulipa deni hilo.

Chalahani anaeleza kuwa'Agizo la kukata maji linatoka kwenye wizara ya maji ambapo waziri aliagiza Mamlaka ikusanye madeni yake yote kutoka taasisi za serikali na watu binafsi na ikishindwa basi mamlaka hiyo itakuwa haipo.

Ameongeza kuwa kinachokosekana Magereza ni mawasiliano ya karibu  kati yao na BAWASA, akiongeza  kwa kusema mbona wenzao Polisi tunawadai na huwa wanakuja mara kwa mara kusema walipofikia?



No comments

Powered by Blogger.