Header Ads

Mjema aungana na yatima, ahimiza upendo


Watanzania wameaswa kuendelea na tabia njema ambazo zilikuwa zinafanywa kwa kipindi cha ramadhani ili kuendeleza upendo amani na utulivu uliko nchini.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema wakati hafla ya iftari aliyoiandaa na kula na watoto yatima ambapo amewataka watanzania kuendeleza upendo ili kutengeneza  jamii iliyo bora

Aidha uadili ni jambi jema hivyo ili uendelee nchini lazima watu wawe kitu kimoja na isiwe mazuri yanayofanywa kipindi hiki cha ramadhani yaishie mwezi huu, kama jamii lazima kuyaendeleza kwani itapelekea kuendeleza upendo miongoni mwetu.


Pia amesisitiza watanzania kushiriki kufanya kazi ili kujipatia kipato kitachopelekea kujenga uchumi ulio imara huku akiwaomba kuliombea taifa pia kumuimbea Rais Magufuli ambae anapigana kuhakikisha amani na upendo unaendelea kudumishwa nchini.


Kwa upande wake Sheikh wa wilaya ya Ilala Adam Kipingu amempongeza Sophia Mjema kwa kitendo cha kuandaa iftari na kula na watoto yatima na waishio katika mazingira magumu kwani ni jambo la kheri na baraka hususani kipindi cha mwezi wa ramadhani.

Ameongeza kuwa ili jamii iwe na upendo lazima ijengwe katika hofu ya mungu ambayo itapelekea kujenga taifa lenye hofu ya mungu.

No comments

Powered by Blogger.