Serikali yatoa onyo kwa wanaowafanyisha kazi watoto
Serikali imepiga vita suala la Ajira kwa watoto wadogo ikiwemo kufanya biashara ndogondogo kwa watoto hao, badala yake wapelekwe shuleni na kuahidi kuwachukulia hatua kali wazazi na walezi watakaokiuka.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Halmashari ya Wilaya ya Tarime Apoo Castro Tindwa kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambapo kiwilaya Wilaya ya Tarime Maadhimisho hayo yuamefanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Nyamongo katika Kata ya Matongo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Apoo Castro Tindwa amepiga vita suala la ajira kwa watoto hususani kufanya biashara ndogo katika Maeneo ya Stendi huku akipiga vita pia suala la Walimu Wa Shule za Sekondari na Msingi kufanya biashara katika Maeneo hayo.
Katika Maadhimisho hayo zimeweza kushiriki Tasisi mbalimbali Likiwemo Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Tarime, ATFGM Masanga, Plan International,Muungano wa Jamii Tanzania MUJATA, Acacia North Mara pamoja na Viongozi wa Dini
Kambibi Kamugisha kutoka Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto na Valerian Mgani kutoka Shirika la ATFGM Masanga wanazidi kupaza sauti zao kwa jamii ili kutokomeza Suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike Wilayani Tarime huku wakiomba serikali Kuungana na Mashirika hayo kwa lengo la kupiga Vita suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa kike.
No comments