Wimbi la watoto wa kike wanaopata ujauzito laongezeka
Idadi ya wanafunzi wanaopata ujauzito wakiwa shule za msingi na sekondari, wakiwa chini ya umri wa miaka 18 imeongezeka katika wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma kutoka 172 mwaka juzi hadi 237 mwaka jana huku vitendo vya unyanyasaji wa watoto na kusomesha watoto wa kiume pekee vikiongezeka.
Afisa ustawi wa jamii katika wilaya ya Buhigwe Petro Mbwanji amesema kutokana na hali hiyo pamoja na kuchukua hatua za kisheria wameweka mikakati ya kutoa elimu na kuunda kamati zitakazokuwa na jukumu la kutokomeza vitendo vya unyanysaji huku muwezeshaji wa Word Vision Tanzania wilayani Buhigwe Metusela Kaganda amesema kutokana na ongezeko wanatoa elimu na kuendesha kampeni za umma vijijini.
Katika wilaya ya Kigoma, mlezi wa kituo cha kulelea watoto Matyazo Mary Leonard amesema baada ya kupokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka halmashauri ya Kigoma, kuwa matokeo ya kutozingatia ushauri juu ya afya ya uzazi umekuwa ukiwaacha watoto wakiwa yatima kutokana na kufiwa na wazazi na kwamba kituo hicho kina watoto wachanga sabini wanaolelewa.

No comments