Shilole Akanusha, ndoa Kumshusha Kimuziki
Msanii wa Bongo Flava, na mwanadada mchakarikaji Shilole amekanusha kuwa hakuna ukweli kuwa kuolewa kwake kunamfanya kushuka kimuziki.Muimbaji huyo akizungumza katika show ya Davido mwishoni mwa wekeend iliyopita amesema amekuwa kimya kutokana ana kazi nyingi nje ya muziki ila sio ndoa.
“Sio kweli, mimi ningekuwa nimepungua kwenye game usingenifanyia interview sasa hivi. Sio kweli nina kazi nyingi za kuniingizia fedha kuliko muziki,” alisema Shilole.
Tangu Shilole aipoolewa December 06, 2017 hajatoa wimbo wowote, wimbo wake wa mwisho kutoa unaitwa Kigori ambao ulitoka August 07, 2017.
Nikujuze usichokijua kuwa Licha ya mwanadada Shilole kuwa msanii kwa upande wa pili wa sarafu ni mjasiriamali ambae anamilikia mgahawa wa chakula maarufu mjini Dar es salaam unaoitwa ‘Shishi Food’, na bidhaa za Shishichili.


No comments