Jeshi la ushirika dhidi ya Daesh lakiri wanajeshi wa Ufaransa kushirikiana na Magaidi
Jeshi la ushiriki linaloongozwa na jeshi la Marekani katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh lakiri kuwa wanajeshi wa Ufaransa wameshirikiana na wanamgambo wa kundi la PKK/YPG Dashicha nchini Syria.
Picha zilizonaswa wakati wa shambulizi la kombora la jeshi la Ufaransa dhidi ya wanamgambo wa Daesh zilisambazwa katika ukurasa wa Twitter wa jeshi la ushirika.
Shirika la habari la Anadolu la Uturuki lilifahamisha Machi 30 kuwa wanajeshi 70 wa Ufaransa walikuwa wakishirikiana na kundi la wanagambo wa PKK/YPG nchini Syria.

No comments