Waziri ampiga STOP kigogo DAWASA
Waziri wa Maji na Umwagiliaji (Eng) Isack Kamwele amemsimamisha kazi Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi, Romanus Mwang'ingo kwa tuhuma za ubadhirifu na udanganyifu katika utekelezaji wa mradi wa kuchimba visima maeneno ya Kimbiji na Mpera huko Kigamboni, Jijini Dar es salam.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Eng. Kamwelwe amesema hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi wa taarifa ya kuwepo kwa udanganyifu na ubadhirifu katika utekelezaji wa mradi wa kuchimba visima vya maji Kimbiji na Mpera huko Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Aidha Taarifa ya Waziri Kamwele imesema kuwa kutokana na kuwa Mhandisi Mwang'ingo ndiye aliyekuwa Msimamizi Mkuu wa mradi huo kwa niaba ya DAWASA na seerikali basi anatengua nafasi yae hiyo ili kupisha uchunguzi wa TAKUKURU.
Aidha Waziri amemteua Dkt. Sufian Masasa kukaimu nafasi hiyo mpaka utaratibu mwingine utakapokamilika.
Mbali na kutengua nafasi ya Afisa hiyo.
Pamoja na hayo Waziri Kamwele amevunja Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA kwa kushindwa kuchukua hatua mapema katika kunusuru mradi huo.
No comments