Header Ads

Wenyeviti watatu wa Chadema watumbuliwa


NA TIMOTHY ITEMBE TARIME,
CHAMA cha Demokrasia na maendeleo Chadema wilaya Tarime Mkoani Mara kimwatumbua nyadhifa wenyeviti waserikali ya Kijiji cha Nyamwaga ha mwingine wa kitongoji cha Nyamwaga Senya pamona na mjumbe wa serikali wa kijiji mojaKoroso Sai kwa tuhuma mbalimbali za kutumia madaraka yao vibaya.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema  wilaya Tarime.Lukas Ngoto aliwaambia waandishi wa habari kuwa viongozi hao wametumbuliwa na mkutano mkuu wa chadema kata ya Nyamwaga ambao ulihudhuriwa na wanachama kutoka vijiji vyote 05 hapo 13,06,2018.

Ngoto aliwataja waliotumbuliwa kuwa ni Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamwaga,Getende Shangirai Lawi mwenyekiti wa mtaa Nyamwaga Senta,Mniko Chacha Magori pamoja na mjumbe wa serikali wa kijiji hicho,anayejulikana kwa jina la Koroso Sasi.

"Chama kinatoa wito kwa viongozi ngazi mbalimbali ndani ya chama wilaya Tarime ili kuendelea kuwatumikia wananchi kwasababu waliomba nafasi hizo huku wakijinadi kuwa watatenda haki katika kuwatumikia siovinginevyo"alisema Ngoto.

Kwa upande wake diwani kata ya Nyamwaga,Yomani Misiwa Chadema ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya Tarime vijijini alisema kuwa viongozi hao wamechukuliwa hatua na chama kutokana na tuhuma za kutumia madaraka waliopewa na wanachi vibaya ikiwemo kutiuhumiwa kukigawa chama katika makundi makundi.

"Viongozi hao wamevuliwa uwanachama pamoja na nyadhifa zao ndani ya Chama kutokana na sababu ya kukigawa chama makundi makundi,harufu ya wizi kuwa wanatuhumiwa kuiba dumu la maji lita zaidi ya 10,000 na waliohusika kuwavua uwanachama ni wanachama wa Chadema mkutano mkuu wa kata wenye vijiji vitano ambavyo ni Nyamwaga,Komarera,Keisangura,Kimusi pamoja na Gwitare"alisema Misiwa.

Pia Misiwa ameongeza kuwa Chama chake hakitasita kuwachukuliwa hatua mbalimbali viongozi wake ambao wanakiuka utaratibu na kushindwa kuwatumikia wanachi waliowachagua katika maeneo yao ya kazi.



No comments

Powered by Blogger.