Header Ads

Wizkid kutumbuiza katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia


Msanii kutoka Nigeria, Wizkid anatarajiwa kutumbuiza katika ufunguzi wa michuano ya Kombo la Dunia ambayo inaanza leo June 14, 2018 nchini Urusi.

Taarifa kutoka vyanzo mbali mbali vya habari vinaeleza kuwa Wizkid atatumbuiza na wasanii wengine kama Will Smith, Nicky Jam na Era Istrefi ambao wataimba wimbo maalumu kwa ajili ya michuano hiyo.

Michuano hiyo itaanza rasmi kwa ufunguzi wa mchezo kati ya Urusi na Saudia Arabia.

Wasanii wote watatumbuiza dakika 30 kabla ya mchezo huo kuanza ambao unatabiriwa kutazamwa na watu wengi zaidi ulimwenguni. Utakumbuka Wizikid alikuwa ni miongoni mwa wasanii waliokuwa wakihamasisha mashabiki kununua jezi za timu ya taifa ya Nigeria.



No comments

Powered by Blogger.