Header Ads

DALILI KWAMBA MKEO HARIDHIKI NA UTENDAJI WAKO WA KITANDANI

Tendo bora la ndoa linatakiwa kuandamana na uwezo wa mawasiliano yaliyo wazi na bila soni. Lakini, ukiwa miongoni mwa wale wasiokubali mapungufu na mkeo akawa mwenye soni, atasita kukueleza kuwa haridhiki na utendaji wako wa kitandani. Lakini, unaweza kulielewa hilo kupitia njia maalumu au kwa kuangalia ishara zifuatazo:
  1. Utaona anazungumza na watoto kwa ukali kiasi kwamba ukiangalia sababu ya huo ukali huioni.
  2. Utaona matumizi yanaongezeka, huku akizidisha kujinunulia vitu binafsi, badala ya vitu vya wote.
  3. Uzito wake utaongezeka, kwa sababu anakula kwa msukumo wa mihemko.
  4. Atakuonesha ishara ambazo ukiwa pamoja na marafiki zako hakuna anayezielewa tofauti na wewe.
  5. Anakurushia maneno yenye mafumbo kila anapopata fursa.
  6. Anakuwa hana msisimko kitandani, anakuwa baridi kama barafu, atakupa mwili tu, lakini moyo uko sehemu nyingine kabisa.
  7. Utamuona anakosa utulivu mara kwa mara, na wakati mwingine anaweza kuonesha hali ya kuwa na mchecheto.
  8. Huonekani kuwa una jema lolote, anakukosoa kwa kila unalosema na kulifanya


No comments

Powered by Blogger.