MWINYI ZAHERA: HATUNA UTOFAUTI WOWOTE NA WALIOWEKA KAMBI UTURUKI
Kocha Mkuu wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera ameibuka na kusema wao na Simba hawana utofauti kutokana na mafanikio ya kambi ya Morogoro.
Jeuri hiyo imekuja kufuatia kuwalaza Waarabu mabao 2-1 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger kwenye Uwanja wa Taifa juzi.
Zahera anaamini kuwa wao Simba na Azam wana usawa kutokana na kikosi chake kuimarika tofauti na hapo awali kupewa nafasi finyu ya kufanya vema kuelekea Ligi Kuu Bara msimu ujao.
"Tulikuwa na wiki mbili za mazoezi Morogoro kwa sasa timu ilivyo naweza kusema tunaweza kuwa katika usawa na timu zingine kama zile zilizoenda Uturuki na hata Uganda katika ubora''
''Timu sasa imeimarika nafurahi tuna kikosi imara cha kushindana na timu yoyote, wachezaji tuliowaongeza wameleta nguvu na ukiongeza na hawa waliokuwepo timu yetu ipo vizuri" alisema.

No comments