Header Ads

SIMBA HII BALAA TUPU, KIKAO KIZITO CHA BODI YA WAKURUGENZI CHAITISHWA KIMYAKIMYA


Ni dhahiri shahiri Simba wameendelea na mkakati wa kuelekea kukamilisha kwa asilimia 100 mfumo mpya wa uendeshaji baada ya viongozi wa juu kuitisha kikao maalum usiku wa jana.

Kikao hicho cha Bodi ya Wakurugenzi kilichoongozwa na Mwekezaji Mohammed Dewji 'Mo' kilikuwa kinafanyika kujadili masuala mbalimbali ya klabu hiyo ambayo yatakuja kuwekwa hadharani baadaye.

Moja ya mikakati iliyojadiliwa kwenye kikao hicho ni pamoja na mbio za ubingwa kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara 2018/19.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema klabu imeamua kubadilisha mfumo huo kwa ajili ya kutomtegemea mtu mmoja na badala yake itakuwa na mwekezaji.

"Tumebadili muundo wa uendeshaji wa klabu ili kutomtegemea mfadhili, muundo huu unatupa fursa sisi na mwekezaji kuipeleke Simba mbele zaidi, shida ya kumtegemea mtu akisusa au vinginevyo ni shida"

"Sasa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi Simba kinaendelea na lolote linaloamuliwa linafanywa na Bodi na si mtu" alisema.

No comments

Powered by Blogger.