Header Ads

Muda wa Kumuonesha Trafiki Leseni ni Ndani ya Siku 3


Sio kosa kisheria kushindwa kumuonesha Trafiki leseni pale anapoihitaji endapo utakuwa huna leseni yako kwa wakati huo.

Kifungu cha 77(1) cha Sheria ya Usalama Barabarani kinasema kuwa mtu hatatiwa hatiani, kwa maana ya kulipa faini au kuandikiwa kosa au kuadhibiwa na chombo chochote ikiwamo Mahakama, kwasababu tu hakubeba, au hakutoa/kuonesha leseni pale alipotakiwa kufanya hivyo, isipokuwa ana siku tatu za kutoa au kuonesha leseni hiyo tokea siku aliposimamishwa.

Aidha, dereva unashauriwa kupiga picha leseni yako ili angalau uwe na kumbukumbu ya namba ya leseni.


No comments

Powered by Blogger.