Fahamu jinsi ya kuachana na mchepuko ili ubaki njia kuu.
| mchepuko ni dili feki, baki njia kuu |
Habari za muda huu rafiki yangu, bila
shaka u mzima na unaendelea na utaraitibu wako wa kila siku wa kutafuta griss
ili kulaini vile vyuma vilivyokaza.
Na siku ya leo naomba tujifunze kwa
pamoja kuhusu ni kwa namna gani tunaweza kuachana na michepuko, kwani nimekuwa
nikipokea jumbe nyingi sana za wasomaji wangu, wengi wakiniuliza afisa
mipango nifanye nini ili niweze kuachana na mchepuka na kubaki njia kuu?
Nami bila hiana naomba nitirike hapa
siku ya leo ili niwaponye wengi kwani swali la aina hii limekuwa likiwatesa
wengi, kwa sababu wengi wa wanaume au wanawake ambao wanachepuka imekuwa
ni suala gumu sana kuweza kuondoka katika mchepuko na kubaki njia kuu.
Mtego ambao umekuwa unatumiwa na michepuko
kuwanasa wapenzi wa watu wengine, umekuwa upo vizuri kwa sababu pindi watu
wanasapo imekuwa ni ngumu sana kunasuka. Kama na wewe ni miongoni mwa watu hao
ambao wamekuwa wakichepuka na wameshindwa kunasuka unachotakiwa kufanya ni;
1. Unapokuwa upo pamoja na mchepuko
au wahenga wa hivi karibuni huita hawala, unachotakiwa kufanya ni kumsimulia
mchepuko wako mambo mengi mazuri ambayo huwa unafanya uwapo na njia kuu. Kama
hiyo haitoshi msimulie mchepuko kuhusu uzuri wa njia kuu pasipo kuona
aibu wala kukosoa uzuri na ubaya wa njia kuu. Kufanya hivyo itamsaidia mchepuko
huyo ajisikie vibaya kwani michepuko mingi huwa haipendi kusikia habari
zinazohusu njia kuu.
2. Punguza mawasiliano na Mchepuko.
Nafahamu fika wakati unapoanza
mahusiano na huyo ambaye unamuita after baby mawasilino yalikua ni mazuri sana.
Vivyo hivyo kama unataka kuachana na mchepuko wako basi unatakiwa kufanya
ni kufanya kinyume chake, yaani mawasilino yawe ni finyu ikiwezekana yafe
kabisa. Muda mwingine akikupigia simu ona kama umeona moto unaowaka.
Mpaka kufikia hapo si la ziada mwisho
nimalize kwa kusema " Mchepuko ni dili feki, tafadhari baki njia
kuu.
Ndimi: Afisa wa mipango na mafanikio
Benson Chonya
bensonchonya23@gmail.com
No comments