Mkuu wa jeshi la polisi nchini(IGP) Simoni Sirro, amesema tuhuma
zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani kuwa polisi
walihusika kuwatoa nje wasimamizi wa uchaguzi mdogo wa udiwani
uliofanyika hivi karibuni si za kweli kwa sababu hajawahi kupokea barua
ama malalamiko ndani ya ofisi yake kutoka kwa viongozi hao.
IGP Sirro ameyasema hayo mkoani Lindi, wakati akizungumza na waandishi
wa habari na kueleza kwamba tuhuma hizo zinazotolewa na viongozi hao si
za kweli kwani hajawai kupata malalamiko hayo na kusema kuwa kama kuna
mtu ana ushahidi na tukio hilo atoe taarifa mara moja ndani ya jeshi la
polisi ili waweze kupeleleza na kuchukua hatua.
Hata hivyo IGP Sirro akasema jeshi la polisi nchini limejipanga katika
kuhimarisha ulinzi katika sikukuu zote mbili za Noeli na mwaka mpya .
Aidha IGP Sirro mara baada ya kufika mkoani Lindi aliweza kukutana na
kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na pia akatembelea kambi ya kisosi
ya kutuliza ghasia aliweza kuangalia mazoezi mbalimbali yanayofanya na
jeshi la polisi mkoani Lindi.
No comments