FEDHEHA 10 AMBAZO MASHABIKI WA UNITED HAWATAKUJA KUZISAHAU.
Usiku wa December 20, 2017
ulikuwa aibu na majonzi kwa mashabiki wa United baada ya timu yao kutolewa
katika michuano ya Carbao Cup, wengi wanajipa moyo kuwa hawakulihitaji kombe hilo ila kiuhalisia roho zinawauma, tuone matokeo 10 yaliyowahi kuwaumiza
United.
10.Manchester United vs Southampton 1976. Hii ilikuwa fainali ya
michuano ya FA, Southampton hawakupewa nafasi hata kidogo kwani hata maandalizi
yao yalikuwa ya hovyo, lakini siku ya mechi bao pekee la Bobby Stokes
liliizamisha United.
09.Mk Dons vs Manchester United 2014.Hii inakumbukwa sana na
mashabiki wa United ilikuwa August 26, moja ya vitu United walitamani kuviona
ni mchezaji wao mpya Angel Di Maria, Mk Dons ambayo ilitengenezwa na wachezaji
wengi wa chuo waliiadhiri United kwa kuipiga bao 4 kwa nunge.
08.Manchester United vs Leeds 2010.Ilikuwa raundi ya 3 ya
michuano ya FA na atakayepigwa anaondoka, siku ya January 4 hakuna shabiki wa
United aliyekuwa na hofu na vibonde Leeds kwa kuwa walikuwa wakienda Old
Traford lakini United walishangazwa na bao la Jermaine Beckford lililoilaza
United.
07.Bournemouth vs Manchester United 1982.United walipigwa bao 2
ugenini huku wakati huo kocha Harry Reknapp ndio alikuwa akianza anza ukocha
akiwa anaifundisha Bournemouth na baada ya Reknapp kuiua United alikiri kwamba
hiyo ndio ilikuwa siku ya furaha kubwa maishani mwake.
06.Manchester United vs York 1995.David Beckham alikuwepo,
Phill Neville alikuwepo na Paul Scholes alikuwepo na walikuwa Old Traford
lakini bado walishangazwa na timu kutoka daraja la pili York ambao waliichapa
United kwa mabao 3 kwa nunge.
05.Southend vs Manchester United 2006. November 7 mwaka 2006
katika raundi ya nne ya FA, United waliwafuata Southend wanaoonekana ni
vibonde, bao la Southend liliwapa furaha kubwa mashabiki wao kiasi cha kufanya
wachezaji wa United kutolewa uwanjani chini ya ulinzi wa polisi baada ya
mashabiki wa Southend kuvamia uwanja.
04.Manchester United vs Norwich 1967. Hii ilikuwa mwezi
February katika raundi ya 4 ya FA, majina makubwa akiwemo Sir Bobby Charlton
yalitosha kutabiri kwamba Norwich wanakwenda kuchezea kichapo lakini mchezo
ukaisha kwa Norwich kuibuka kidede kwa mabao 2 kwa 1.
03.Manchester vs Middlesbrough 2015. Hii ilikuwa sare ya bila
kufungana katika uwanja wa Old Traford, lakini suluhu hii ilishuhudia United
wakiondolewa katika kombe la ligi kwani tayari mchezo wa kwanza walitoka
kupigwa mabao 3 kwa 1.
02.Manchester United vs Crystal Palace 2011. Robo fainali ya kombe la
ligi mwezi November 2011, Old Traford palionekana panaweza kuwa mwisho wa
Crystal Palace kutokana na nguvu waliyokuwa nayo United lakini bao la dakika za
nyongeza la Glen Murray liliufanya mchezo huo kuisha kwa Palace kuibuka kidedea
kwa bao 2 kwa 1.
01.Bristol vs Manchester United 2017. Hii ndio habari kubwa
wiki hii , ambapo mashabiki wa Manchester United hawakuamini baada ya safari
yao ya EFL Cup kukatishwa na timu ambayo haipo hata ligi kuu kwa mabao 2 kwa 1.

No comments