UCHUNGUZI WA CHANZO CHA MAUAJI YA KIMBARI RWANDA WAKAMILIKA.
Majaji wa Ufaransa wamemaliza upelelezi juu ya shambulio la
kombora ambalo lilisababisha kuanza kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka
1994.
Ofisi ya mwendesha mashitaka sasa wataamua ikiwa waipeleke kesi
mbele ya mahakama. Majaji wamewalaumu wapiganaji walioongozwa na rais wa sasa
wa Rwanda, Paul Kagame kwa kuilenga na kuiangusha ndege iliyokuwa imembeba rais
wa wakati huo wa taifa hilo, Juvenal Habyarimana.
Rwanda nayo inawalaumu Ufaransa kwa kushiriki kupanga mauaji ya
kimbari. Upelelezi umesababisha sintofahamu kati ya mataifa haya mawili, kiasi
cha Rwanda kuvunja uhusiano wa kidplomasi a na ufaransa mwaka 2006.
Uhusiano huo ulirejeshwa miaka mitatu iliyopita.
CHANZO; BBC NEWS

No comments