Habari njema, Serikali yatangaza ajira mpya za walimu
Serikali
imetangaza kutoa ajira mpya za walimu wa shule za msingi na sekondari
hii leo, ambapo jumla ya walimu 3033 wamechaguliwa na kupangiwa vituo
vya kazi.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), Seleiman Jafo, akiongea na waandishi wa habari leo,
ametangaza kuwa walimu wamechaguliwa ili kwenda kuziba nafasi iliyoachwa
wazi na walimu waliobainika kuwa na vyeti feki baada ya zoezi la
uhakiki kukamilika.
“Majina
ya walimu yanayotangazwa leo yanatokana na tangazo la serikali la
kuziba nafasi zilizoachwa wazi kwa walimu katika shule za msingi na
sekondari waliobainika kuwa na vyeti vya kughushi mapema mwaka huu
ambapo mnaklumbuka zoezi hili lilikuwa linafanyika kupitia Ofisi ya Rais
utumishi,” amesema Waziri Selemani Jafo.
Waziri
Jafo ameeleza kuwa kati ya walimu waliopangiwa vituo vya kazi walimu
266 ni wa shule za sekondari na walimu 2767 ni wa shule za msingi na
kuwataka waripoti ndani ya muda uliowekwa ambao ni kuanzia Disemba 27,
207 mpaka Januari 7, 2018 wakiwa na vyeti halisi vya elimu pamoja na
cheti cha kuzaliwa.
“Baada
ya uhakiki wa maombi ya walimu yaliyotumwa serikalini, jumla ya walimu
3033 wamechaguliwa kupangiwa viyo vya kazi. Kati yao walimu 266 ni wa
sekondari na 2767 ni wa shule za msingi. Walimu hao wanatakiwa kuripoti
katika Walimu hao wanatakiwa kuripoti kuanzia tarehe 27 Disemba 2017
hadi Januari 7, 2018 wakiwa na mahitaji yafuatayo. Wawe na vyeti halisi
vya taaluma ya kidato cha tano na cha sita, awe na cheti cha kitaaluima
cha kuhitimu mafunzo ya ualimu kwa ngazi husika na mwish awe na cheti
cha kuzaliwa,” amesema Jafo.
Aidha
amewatahadharisha waajiriwa wapya kuhakikisha kuwa wanaripoti katika
vituo walivyopangiwa kwa wakati na kuwaonya kutohama vituo vyao vya kazi
pasipo kupata ridhaa kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI.
“Waajiriwa
wapya wanatahadharishwa kuriporti katika shule husika na hatutarajii
mtu mmoja kuhama kutoka shule moja na kwenda nyingine ndani ya
halmashauri au mkoa wake bila ridhaa ya Ofisi ya Rais TAMISEMI,” alionya
Waziri Jafo.
No comments