KANISA LA UKOMBOZI LATEMBELEA KITUO CHA AMANI, LAKUMBUSHA KUJALI WATOTO
WATANZANIA
wamekumbushwa kuwajali na kuwangaalia watoto yatima na wale wanaoishi
katika mazingira magumu kwa kuwatimizia mahitaji yao ya kimwili na
kiroho. Aidha, wamepaswa kutambua kwamba wana wajibu wa kusaidia watoto
hao kwa kuwa wanawekeza kwa manufaa ya taifa na wao wenyewe. Kauli hiyo
imetolewa na Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa
Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, akizungumza baada ya kukabidhi
vifaa, bidhaa na mahitaji mbalimbali ya watoto yatima wa kituo cha
Amani, kilichopo Bagamoyo, kiasi cha kilomita 65 kutoka Dar es salaam.
na
Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko (mwenye gauni la
bluu) wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akizungumza jambo mara
baada ya kuwasili kwenye ofisi za Mkurugenzi wa kituo cha kulelea
watoto yatima cha Amani, Margareth Mwegalawa (katikati) kukabidhi vitu
mbalimbali kituoni hapo akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa
kanisa, waumini na wamama.
Akitoa maneno yanayogusa nyoyo huku akikariri maandiko Mchungaji Faith alisema:“Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu baba ni hii, kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa” Alifafanua kwamba Kanisa lisiloangalia yatima na wajane si Kanisa, alisema na kuongeza kuwa waumini wanastahili kuwajibika kwa hilo. Aidha, alisema kama Kanisa wanajali watoto na ndio maana wamefunga safari kwenda kuwaona na wamefurahi kuwaona na kushiriki nao tafrija fupi baada ya kuwakabidhi zawadi mbalimbali.
na Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko (wa kwanza kulia)
wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam na baadhi ya viongozi,
wakinamama na waumini wakifungua tafrija hiyo fupi kwa maombi kabla ya
kukabidhi mahitaji mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima
kilichopo kijiji cha Zinga, Bagamoyo.[/caption] Waumini wa kanisa hilo
walikabidhi mahitaji ya shule ya watoto, mavazi na chakula. Aliwataka
watanzania kuwa na tabia ya kujali watoto hao kwa kuhakikisha wanapata
mahitaji yao kila siku na sio siku ya sikukuu tu. Alisema watoaji
wanapaswa kutoa kwa hali na mali kwa ajili ya kuondoa dhiki za watoto
hao, ikiwa ni sehemu ya Baraka kamili kwa Mungu na pia kwa taifa.
Alisema watoto hao hawajulikani kesho watakuwa watu gani na kama
watalelewa vyema watakuwa ni sehemu ya taifa lenye uadilifu na woga kwa
Mungu. [caption id="attachment_3424" align="aligncenter" width="1404"]
Baadhi ya wakinamama wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam
wakishiriki maombi baada ya kuwasili kwenye kituo cha kulelea watoto
yatima cha Amani kilichopo katika kijiji cha Zinga, mjini
Bagamoyo.[/caption] Alisema kwa kuwezesha utulivu wa watoto hao, watoto
watamjua Mungu na hivyo kujenga taifa lenye maisha yenye utukufu wa
Mungu. Naye, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Esther Pilila alisema
kwamba kama wanawake katika Kanisa lao wamesukumwa na haja ya
kuwaangalia watoto hao kama wajibu wao. Akizungumza kushukuru Mkurugenzi
wa kituo hicho Margareth Mwegalawa aliomba watanzania kuwakumbuka
watoto hao na kuitafadhalisha serikali kuwapitia kila mara kwa kuwa wao
ndio walezi wa watoto.
Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la
Ukombozi tawi la Dar es Salaam akisaini daftari la wageni alipowasili
katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Amani kilichopo katika kijiji
cha Zinga, Bagamoyo.
Akitoa maneno yanayogusa nyoyo huku akikariri maandiko Mchungaji Faith alisema:“Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu baba ni hii, kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa” Alifafanua kwamba Kanisa lisiloangalia yatima na wajane si Kanisa, alisema na kuongeza kuwa waumini wanastahili kuwajibika kwa hilo. Aidha, alisema kama Kanisa wanajali watoto na ndio maana wamefunga safari kwenda kuwaona na wamefurahi kuwaona na kushiriki nao tafrija fupi baada ya kuwakabidhi zawadi mbalimbali.
Alisema
pamoja na chakula walichopewa wanatamani watu mbalimbali kuendelea
kuwajali watoto kwa kuhakikisha wanakuwa salama. Alisema wadau
mbalimbali wasiangalie tu vituo vya mashirika ya dini bali vituo vyote
ambavyo vinabeba mzigo wa malezi kwa watoto yatima na wale wanaoishi
katika mazingira hatarishi. Alisema kituo cha Amani chenye watoto 40
kinahitaji kupata uzio ili kuhakikisha watoto wapo salama.
Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la
Ukombozi tawi la Dar es Salaam akiwa amempakata mtoto Nicolaus (1.5)
wakati wakitazama burudani kutoka kwa watoto wa kituo cha kulelea yatima
cha Amani kilichopo katika kijiji cha Zinga, Bagamoyo.
Naye
mtoto Salama Ismail (12) alishukuru kwa misaada hiyo ya mavazi na
chakula, mafuta ya kupakaa, miswaki na madaftari na kutaka wananchi
wamjue Mungu kwa kuwajali. Naye Haji Joseph (11) aliomba viongozi wa
serikali kuwatembelea kwani wao ndio wazazi wao na kuwasaidia kuimarisha
upatinakaji wa nishati katika kituo chao hasa umeme wa REA. “Tunaomba
viongozi wa serikali watutembelee tuwajue na hasa Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa” alisema mtoto huyo.
Watoto wa kituo cha kulelea yatima cha Amani kilichopo Zinga, Bagamoyo
wakitoa burudani sambamba na Mkurugenzi wa kituo hicho Margareth
Mwegalawa walipotembelewa na waumini wa kanisa la Ukombozi wakiongozwa
na Mchungaji Faith Tetemeko (hawapo pichani) wakati wa tafrija fupi ya
kukabidhiwa mahitaji mbalimbali ya kujikumu kituoni hapo.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wakinamama wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam walioshiriki tafrija hiyo.
Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko (mwenye gauni la
bluu) wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akicheza sambamba na
mtoto Haji Joseph (11) katika tafrija fupi ambapo Kanisa la Ukombozi
lilikabidhi vitu mbalimbali zikiwemo sare za shule, vyakula, madaftari,
nguo na mahitaji mengine ya kujikimu.
Pichani juu na chini ni wakinamama wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es
Salaam wakiwa wamebeba vitu mbalimbali vilivyotolewa kwenye kituo cha
watoto yatima cha Amani kilichopo Zinga, Bagamoyo.
Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko (katikati) wa Kanisa
la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akikabidhi vifaa, bidhaa na mahitaji
mbalimbali ya watoto wa kituo cha Amani cha watoto yatima, kilichopo
Bagamoyo kwa Mkurugenzi wa kituo hicho Bi. Margareth Mwegalawa (kulia)
katika hafla fupi iliyofanyika kituoni hapo Bagamoyo. Kushoto ni ,
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Kanisa la Ukombozi tawil la Dar es
Salaam, Esther Pilila.
Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la
Ukombozi tawi la Dar es Salaam katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa kanisa hilo, watoto pamoja na walezi wa kituo hicho
Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la
Ukombozi tawi la Dar es Salaam katika picha ya pamoja na wakinamama wa
kanisa hilo na walezi wa kituo hicho mara baada ya kukabidhi msaada huo.
Mwalimu Heavenlight (kushoto) na Mwanaukombozi Favour wakipozi na mtoto Nicolaus (1.5) kuonyesha upendo kwa mtoto huyo
Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la
Ukombozi tawi la Dar es Salaam akigawa chakula kwa watoto yatima wa
kituo cha Amani kilichopo Bagamoyo mara baada ya kukabidhi vitu
mbalimbali kituo hapo.
Watoto yatima wa kituo cha Amani kilichopo Bagamoyo wakifurahia chakula
cha pamoja kilichoandaliwa na wakinamama wa kanisa la Ukombozi tawi la
Dar es Salaam.
Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la
Ukombozi tawi la Dar es Salaam akishiriki chakula cha pamoja na watoto
yatima wa kituo cha Amani kilichopo Bagamoyo.
Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la
Ukombozi tawi la Dar es Salaam akimlisha chakula mmoja wa watoto yatima
wa kituo cha Amani kilichopo Bagamoyo mara baada zoezi la kukabidhi
misaada mbalimbali kituoni hapo.
Pichani juu na chini ni Wakinamama wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es
Salaam wakicheza michezo mbalimbali na watoto yatima wa kituo cha Amani
ukiwemo 'Tulinge Baiyoyo' mchezo ambao katika makuzi kila mtu
aliupitia.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es
Salaam, Esther Pilila akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa kituo hicho
mara baada ya kuhitimisha zoezi la kukabidhi msaada huo.
Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la
Ukombozi tawi la Dar es Salaam akizungumza na kituo cha televisheni cha
Channel Ten mara baada ya kukabidhi misaada hiyo kituoni hapo.
Mtoto Haji Joseph (11) wa kituo cha watoto yatima Amani akitoa neno la
shukrani kwa kanisa la Ukombozi kwa kupokea misaada hiyo katika tafrija
fupi iliyofanyika kituoni hapo.
Mtoto Salama Ismail (12) wa kituo cha watoto yatima cha Amani akitoa
shukrani kwa misaada hiyo ya mavazi na chakula, mafuta ya kupakaa,
miswaki na madaftari iliyotolewa na wakinamama wa kanisa la Ukombozi
tawi la Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha Amani kilichopo Bagamoyo, Bi.
Margareth Mwegalawa akisisitiza jambo wakati wa mahojiano na waandishi
wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupokea msaada huo.

No comments