SEMINA YA KUWAJENGEA UWEZO VIONGOZI WA SERIKALI, DINI NA WASIMAMIZI MPANGO WA PETS WAFUNGULIWA SAME
Mkuu wa Wilaya
ya Same, Rosemary Senyamule (wa nne toka kushoto) akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa serikali, dini na wasimamizi wa mpango wa "Public
Expenditure Tracking System" (PETS) waliohudhuria semina iliyofanyika
Same kwa kuwezeshwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).
Na Kajunason/MMG.
Mkuu wa Wilaya
ya Same, Rosemary Senyamule amewataka wasimamizi wa mpango wa
Ufuatiliaji wa Matumizi ya Umma (PETS) kuwa na uadilifu katika
kufiatilia matumizi ya fedha za serikali.
Hayo
ameyazungumza leo wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo
uliowakutanisha viongozi wa serikali, dini na wasimamizi wa mpango wa
"Public Expenditure Tracking System" (PETS) uliofanyika Same kwa
kuwezeshwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).
Mhe. Senyamule
alisema ni vyema watendaji hao wakafuata misingi imara itakayowezesha
serikali kujua ni wapi wanamatumizi mabovu ya fedha katika halmashauli.
Aliagiza
halmashauri kushirikiana kwa karibu na watu hao kwani kazi wanayoifanya
ni ya halmashauri, hasa ukaguzi na mipango. "Idara ya ukaguzi ina
watumishi 3 tu wanaohitaji kukagua kila kitu, sio rahisi wakidhi kwa
wakati; lazima tuwashirikishe wadau wa PETS ili taarifa zao ziwe ni moja
ya misingi ya ufuatiliaji kwa halmashauri," alisema Mhe. Senyamule.
Pamoja na yote Mhe. Senyamule aliomba CCT kuongeza idadi ya kata wanazofanyia kazi kutoka 11 hadi zote 34 zilizopo kwa sasa.

No comments