Michezo miwili ya kombe la Azam Sports Federation Cup (FA Cup)
imeshindwa kuchezwa jijini Dar es Salaam kwa sababu ya wachezaji kukosa
leseni za kufanyia kazi hivyo mechi hizo zimeahirishwa hadi TFF
itakapotoa mwongozo juu ya suala hilo.
Mchezo wa Abajalo vs Tanzania Prisons (uwanja wa Uhuru) umeshindwa
kuchezwa baada ya wachezaji zaidi ya watano wa Abajalo kugundulika kuwa
hawana leseni za kuwaruhusu kucheza mashindano.
Mchezo mwingine ambao haujachezwa kwa sababu ya wachezaji kukosa lesini
ni kati ya Mvuvumwa dhidi ya JKT Ruvu (uwanja wa Azam Complex).
Katibu mkuu wa Tanzania Prisons Havinitishi Abdallah amethibitisha
kwamba mchezo huo haujachezwa na wao wanasubiri kusikia TFF inasemaje
kwa kile ambacho kimetokea kwenye mchezo wao dhidi ya Abajalo.
“Hatujacheza kwa sababu wachezaji kama saba wa Abajalo hawakuwa na
leseni, tunasubiri kusikia kutoka TFF kwa sababu wao ndio wanazitoa,
baada ya hapo ndio tutajua tuseme nini lakini kwa sasa hatuwezi kuongea
chochote.”
No comments