Picha : POLISI SHINYANGA YAKAMATA GARI LENYE MITAMBO YA MINARA YA SIMU ILIYOIBIWA VODACOM
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata gari lenye namba
za usajili T.243 CVU Toyota Carina mali ya Mayeka Mlenda mkazi wa
Kahama likiwa limebeba mali za wizi ikiwemo betri 9 za minara ya
mawasiliano ya simu ya kampuni ya Vodacom.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule
alisema mali hizo zimekamatwa kupitia operesheni mbalimbali
zinazoendelea likihusisha taarifa za kiintelijensia.
Alisema gari hilo lilikamatwa likiwa na betri kubwa 9 za minara ya
mawasiliano aina ya North Star,betri moja ya jenereta aina ya Koba N70
na Copper wire Cable mbili zenye urefu wa mita 28 vinavyokadiriwa kuwa
na thamani ya shilingi 12,338,000/= mali ya kampuni ya simu ya Vodacom.
Kufuatia tukio hilo watuhumiwa walikimbia na kulitelekeza gari.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule akionesha waandishi wa
habari mali za wizi zilizokamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga
vilivyokuwa kwenye gari pichani ambazo ni betri na waya - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Waandishi wa habari wakiangalia mali za wizi zilizokamatwa na polisi Shinyanga
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule akionesha gari lililokamatwa na mali za wizi
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule akifungua mlango wa gari
lililokamatwa na mali za wizi mali ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog





No comments