Fid Q atunukiwa Tuzo ya Heshima
Hip Hop Icon, Legend Kwenye Bong Hip Hop Farid Kuband a.k.a fid q ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Kuiwakilisha Vyema Kanda ya Ziwa Kupitia Muziki Anaoufanya.
Kupitia Ukurasa Wake wa Instagram Rapa Huyo ameandika kuwa Amepokea Tuzo Hiyo Kutoka Kwa Wataalam wa Masuala ya Mazingira wanaoitwa Kijani Consult Tz ikiwa ni sehemu ya Mchango wake katika kuiwakilisha Vyema Kanda ya Ziwa Kupitia Sanaa ya Muziki.
Fid Q Mwenye Hit Songs Kibao ameshukuru kwa watoaji wa Tuzo hiyo na ameshukuru Pia Mashabiki Zake kwa Kuweza Kufanikisha Swala Hilo.


No comments