Kura kubaini walimu wanao watomasa wanafunzi
SERIKALI wilayani Nkasi mkoani Rukwa imetangaza kuwa kura za maoni zitapigwa katika shule zote za msingi na sekondari ili kuwabaini walimu wenye tabia ya kuwapapasa wanafunzi wa kike na viongozi na madereva wa bodaboda wenye tabia za ukware ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika kimkoa mjini Namanyere. Sambamba na hilo, pia wanafunzi watapiga kura za maoni ili kuwabaini wanafunzi wenye uhusiano ya kimapenzi baina yao.
“Wanafunzi watakaobainika kuwa na uhusiano wa kimapenzi baina yao wenyewe kupitia kura ya maoni adhabu yake itakuwa kila mmoja kucharazwa viboko sita,” alisema. Alikitaka Chama cha Walimu (CWT) wilayani humo kisiwakingie kifua walimu watakaobainika kuwa wakware shuleni kwa kuwa wakali kikitoa madai kuwa walimu wao wananyanyaswa, badala yake kiunge mkono serikali katika kampeni yake ya kuhakikisha kuwa mtoto anakuwa salama wakati wote.
“Wanafunzi hususani wa kike msikae kimya na kuogopa kusema pale walimu wenu wanapowapapasa, akitokea mwalimu mwenye tabia kama hiyo nendeni kwa Mkuu wa Shule au Mwalimu Mkuu mtoe taarifa .... Wasipowasikiliza na kuchukua hatua dhidi ya walimu hao nendeni kwa diwani wenu, pia kwa Mkuu wa Wilaya milango iko wazi,” alisisitiza.

No comments